Sunday, January 24, 2010

Ajali makutano ya Barabara ya Kawawa na Nyerere asubuhi hii!


Ajali imetokea pale makutano ya Barabara ya Nyerere na Kawawa asubuhi hii baada ya lori hili kufeli likikata kona na kupinduka. Lakini hakuna aliyekufa, ila limesababisha bonge la foleni!

African Stars Band (Twanga Pepeta) Ndani ya Bonanza J'Pili


Twanga wakikamua kwenye viwanja vya wastaarabu vya Leaders Club kwenye bonanza linalodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro

Mama Dotinata ndani ya Leaders Club



Mama Dotinata na pacha wake kama kawaida alikuwepo pia viwanjani hapo akipata burudani ya vijana wa Twanga Pepeta.


Ona hinye onaaaa...Ebwanaaaeeee! Ebwana ingawa sijaziweka hizo picha za hinye lakini Leaders Club siku za jumapili kwenye Bonanza linaloandaliwa na bia ya Kili si mchezo! Maana kunajaa umati wa watu, flowers za kumwaga na hivyo vivazi ndio usiombe! pichani niko na Dj Shorty na Dorica Mshindi wa Tuzo ya Zanzibar Music Award mwaka jana tukifuatilia kila kinachoendelea viwanjani hapo.

Friday, January 22, 2010

Mzee wa alambaa alambaa....ammmmh!



Bado sijajua Mzee Yussuf anamaanisha nini anapoimba alambaaa lambaaa...!!!

Mjomba Mpoto...



Nikipata nauli...nitakuja mjomba

Fm Academia kazi ipo...




Wanenguaji wa Fm Academia



Wanenguaji machachari wa Bendi ya Wazee wa Mujini, Wazee wa Ngwasuma, Wazee wa Bling Bling wakiwa kazini. Jamaa wanakamua kinoma. BIG UP!

Mambo ya Habiba Ntimizi


Bling Bling wa leo!



Mmemuona Tuma.. shingoni amesheheni madini! Si UFISADI huu jamani?

Kilimo kwanza



Tour ya Kipalang'anda - Mkuranga kwa ajili ya kutekeleza sera ya Kilimo kwanza. Umeona eneo hilo?

Wednesday, January 20, 2010

Lauma M. Lauma


Nakumbuka nyumbani, ugali kwa mlenda.