Monday, August 9, 2010

Happy Birthday Cleopatra Kato Rutasitara!!!!!


Patra akiwa katika tabasamu la kukata na shoka kusheherekea sherehe ya siku yake ya kuzaliwa
(miaka mitatu) Hongera Bwana na Bibi Kato kwa kukuza!!!




                                            
  Patra akiwa amebebwa na mama yake (Belinda)

Bwana Kato (aliyetupa mgongo na fulana jekundu) akiwa na wageni waalikwa wakipata kilaji na kubadilisha mawazo kwenye sherehe ya Patra


Bwana na Bibi Kato wakiwa katika picha ya pamoja na Binti yao Patra



Bagamoyo trip!


Friday, June 4, 2010

MSIBA! MSIBA! MSIBA!

Ina lil laahi wa inna ilayhi rajjoun..Habari zilizotufikia alfajiri na mapema ni kwamba Bwana Yusuf Alley (Maarufu Bwana Chuchu) amefariki dunia!  Alikuwa ni shujaa..Mwana Harakati, Mjasiriamali na Mtu wa watu. Mwili unasafirishwa leo kutoka Nairobi alikofia wakati anahangaika kupigania maisha yake kwenda nyumbani kwake Unguja. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo hivi huko Unguja. Taarifa zaidi baadae. Allah aiweke vema roho yake mahala pema peponi Amina!

Tuesday, May 4, 2010

Dar Mpaka Moro

Jamani Morogoro kuzuri.. hali ya hewa na mandhari ya kuvutia..Unaona ukungu milimani? Natamani kila weekend nitembelee sehemu hii!

Greda ikitoa msaada!

Umeona hapo chini ya barabara? Ukinasa hadi greda zije kukunasua!

Kasheshe la Usafiri mikoa ya Kusini

Mdau Exavier kutoka Arusha amenitumia picha hizi alizozipiga karibuni zinazoonyesha kipande ambacho barabara kwenda mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara) kinavyosumbua. Magari mengi hunasa na kusababusha usumbufu kwa wasafiri.

Friday, April 23, 2010

Hapa ni baada ya Mechi kwisha mashabiki wa Yanga wamekimbia uwanjani

Monday, April 19, 2010

Mdau anaomba Mawazo!!

As salaam aleyikum! Tumsifu Yesu Kristu! Bwana Yesu Asifiwe sana! Habari wadau wangu wa Blogu hii: Nilipata kupigiwa simu na mdau mmoja kutoka Songea, yeye ni rafiki yangu na nilikuwa nae pamoja shule O-level pale Ndanda Sekondari!
Alinipa kisa ambacho kama vile alikuwa ananiomba ushauri kwani yupo kwenye dilemma na nikamwambia ni bora nikiandike kwenye blog yangu ili watu wamsaidie mawazo naye akaridhia. Kisa chenyewe ni hiki kifuatacho;
Yeye alikuwa na rafiki wa kike (girl friend) hapo zamani kidogo wakati anasoma o-level, rafiki ambaye alikuwa anampenda sana na mpaka sasa kwa kuwa alishindwa kumsahau amebaini kuwa  ndiye mwanamke anayempenda kuliko mwanamke yeyote aliyewahi kukutana nae maishani mwake. Rafiki yangu ni mwafrika pyua na yule msichana wake ni mchanganyiko wa kiarabu na kiafrika. Walikuwa wanaendelea na urafiki wao na yeye anadai alikuwa hakosi kwenda likizo kwao kwa kuhofia kumuudhi huyo rafikiye wa kike!
Walipishana miaka miwili kimadarasa ina maana wakati jamaa anamaliza kidato cha nne rafiki yake alikuwa kidato cha pili.
Urafiki wao ulikuwa kiasi kwamba hata familia zote mbili zilijua. Tatizo lilikuwa ni upande wa Mwanamke ambaye baba yake (mzee tajiri wa kiarabu) hakupenda kabisaaa jamaa awe ni mchumba kwa binti yake akiamini binti yake bado ni mdogo na haamini kama yale yalikuwa maamuzi sahihi kwa binti yake na pia mwanaume mwenyewe ni maskini wa kiafrika!
Binti hakujali, alionyesha msimamo wa hali ya juu kwa baba yake ikafikia mpaka jamaa aliwekwa ndani na baba yake yule binti kama vitisho tu ili aachane na binti yake!
Jamaa hali ilivyokuwa ngumu ilibidi ahame mji na kwenda mji mwingine wa mbali kutafuta maisha. Lakini baada ya miaka mitatu jamaa alirejea kwao na kupata tu taarifa kuwa yule mpenzi wake (yaani binti wa kiarabu) ameshaolewa na kijana wa kiarabu wapo Arusha. (ikumbukwe kipindi hicho mawasiliano kwa simu za viganjani ilikuwa ni kwa mafisadi tu) kwa hiyo jamaa alipoteza mawasiliano yote na yule dada.
Jamaa naye hakukaa sana kijijini aliamua kwenda Songea mjini kujiendeleza kimaisha! Miaka kumi sasa tangu mkasa huo utokee... Mengi yamefanyika! Jamaa alijiendeleza kishule na kupata taaluma nzuri na kazi nzuri na akafanikiwa kuoa na ana mtoto mmoja.
Wakati wa likizo yake ya Mwaka jana alipotembelea kijijini kwao kusalimia wazazi ndugu jamaa na marafiki aliambiwa pia yule mpenzi wake wa kiarabu alifika kwa ajili ya mazishi ya baba yake mzazi. Na pia alipata maelezo kuwa yule binti alienda mpaka kwa wazazi wa mshkaji kusalimia, aliongea sana na dada wa mshakaji na kuwaambia ni jinsi gani anavyomkumbuka na kumpenda mshkaji na ingawa mume aliyemuoa amezaa nae watoto wawili, na anamjali kwa hali na mali lakini sio chaguo lake!
Baada ya kupata maelezo hayo jamaa alipewa mpaka namba ya simu ambayo yule girl friend wake wa zamani aliiacha ili jamaa akija apatiwe wawasiliane, lakini jamaa aliichukua ile namba na alishindwa kuipiga kutokana na moyo wake kuwa mzito.
Likizo ya mwaka huu jamaa alienda tena kijijini peke yake na akafanikiwa kukutana na yule msichana wake wa kiarabu, kumbe naye alikuja kusalimia. Na safari hii jamaa alienda likizo peke yake bila familia yake, na yule binti naye alikwenda peke yake bila mumewe na wakakutana bila kupanga!
Ilikuwa ni huzuni sana kwa jamaa, kwani walipokutana wote walilia sana. Jamaa anakubali kuwa anampenda sana yule binti ambaye ni mke wa mtu sasa, na yule binti bado anampenda sana jamaa ambaye sasa ni mume wa mtu!(ngoma droo). Kasheshe ni kwamba mwanamke akija pale kijijini anashinda nyumbani kwa jamaa na anasaidia kazi zote za nyumbani akishawishi jamaa kwamba yeye yupo tayari aachane na mumewe yule wa kiarabu ili aolewe na jamaa. Na jamaa anakiri kuwa kweli anampenda huyu msichana na kikwazo kilikuwa mzee wake ambaye sasa ni marehemu, lakini yeye ameshaoa na mkewe hajawahi kumtendea kosa lolote na wana mtoto na wameshafanya vitu vingi vya maendeleo, wamejenga wana magari na vitega uchumi kadhaa kwa muda mchache tu baada ya kuoana.
Yule msicha anasisitiza mbona yeye ameolewa na yupo tayari aachane na mume wake? basi kama yeye hawezi kuachana na mke wake basi yeye yupo tayari kuwa mke wa pili!!!!!!! yaaani jamaa asiachane na mkewe ila yule mwanamke yupo tayari aachane na mumewe ili awe mke wa pili kwa jamaa.
Jamaa hayupo tayari kuwa na wake wawili, ni kweli yule msichana anampenda zaidi kuliko mke aliyenaye. Lakini pia mke wake hana hatia na hajawahi kumkosea hata siku moja katika maisha yake!! Jamaa amechanganyikiwa na hajui afanye nini. Wadau msaidieni. Na majibu ya mawazo yetu tumeni kupitia blogu hii ili kumsaidia.
Natanguliza shukrani!

New Seatbelt Design: 45% less car accidents!!

Monday, April 12, 2010

Nasaha kutoka kwa Bi Kidude

Bi. Kidude akitoa nasaha mbili tatu kwa wajukuu zake ambao hawachoki kumsikiliza kutokana na ufundi wake wa kuzungumza! Hivi sasa Bibi huyu anatamba sana kwenye single ya AHMADA aliyoshikirikishwa na Vijana wa Offside Trick.

Kingwendu mzee wa mistari...


Show zote kwa hisani ya Inachuchu (Sasa Taff Promotion) wataalam wa Burudani Unguja Mzima

2Berry

Kipindi hicho wakiwa pamoja kabla ya kuparaganyika!

Wadau wa Burudani wakifuatilia kwa umakini show huko Unguja.

Style na Miondoko mbalimbali za Rusharoho Unguja!

Kazi si ndogo hii, maana lazima kijasho kiwatoke!

Hii Rusha Roho au Toa Roho?

Mambo ya viuno

Dada anashika ukuta, kaka anashika kiuno!

Sasa hii kali zaidi!!

Duh!

Ebwanaa eeee!

Jamani, sijui ni mzuka au karaha.. Maana Unguja siku hizi taarabu haliwi tamu mpaka watu wacheze hivi. Nimefuatilia maonesho mengi kisiwani hapa yanayofanyika pale Ngome Kongwe na Ukumbi wa Mafunzo na watu hurusha roho kwa namna hii!!!!!!!!

Tuesday, April 6, 2010

Bwa-Chuchu na Forodhani

Unamkumbuka Bwana Chuchu? anaonekana kwa mbali maeneo ya Forodhani akiwa katika jitihada za kuongeza shavu. Bwana Yusuf Alley (Maarufu Bwana Chuchu) ni miongoni mwa vijana wajasiriamali walio mstari wa mbele katika kujenga nchi. Yeye ni mmiliki na Mkurugenzi wa kituo maarufu cha redio cha Chuchu fm (90.9fm) mjini Unguja, Taff Promotion (wataalam wa Burudani -zamani Inachuchu) na ana caffee zake pale Forodhani zinazotoa huduma safi za chakula na vinywaji. Tunakutakia kila la kheri kwa juhudi zako ambazo zinaleta tija kwako, kwa familia yako, ajira kwa vijana, jamii na Taifa kwa ujumla. Karibu Urojo...

Forodhani Tambarare

Muonekano wa Beach maeneo ya Forodhani mjini Unguja. Ukweli panapendeza sana.

Gati ya Abiria Unguja

Gati ya abiria Mjini unguja.. tulikuwa huko kipindi cha sikukuu ya Pasaka

Flowers za Tanzania Printers

Habiba Ntimizi akiwa Angela B. Kessy designer wa Tanzania Printers

Smile la Habiba Ntimizi

Tuma na PASAKA!

Thursday, March 25, 2010

Flower of the Day!

Hili ndilo tembo (pombe ya Mnazi)

Hapa ndio halijatiwa maji kabisa halafu ukilionja linakuwa taaamu! wakimaliza hapa linatiwa maji kidogo ili lichache na kuwa pombe! KARIBU.

Mtambo wa kutengeneza gongo

Wadau mmeona? picha imepigwa kwa kutumia iPhone lakini kwa mbali kidogo kutoka kwa mdau wa Masasi, watu hulazimika kupika na kuuza gongo na kipato huwasaidia kwa mahitaji ya kila siku na kusomeshea watoto!!!!!

Wednesday, March 24, 2010

NINAWAOMBA RADHI WATU WOTE WANAOITEMBELEA BLOG YANGU KUWA KARIBU MIEZI MIWILI SIKUWA HEWANI. HII NI KUTOKANA NA SABABU AMBAZO ZILIKUWA NJE YA UWEZO WANGU, NILIKUWA LIKIZO MAENEO AMBAKO HAKUNA INTANETI. LAKINI NILIPIGIGA PICHA NYINGI SANA SAFARINI ILA NIKAPATA BAHATI MBAYA YA MEMORY CARD YA KAMERA KUHARIBIKA NA KUSHINDWA KUPATA PICHA ZOTE. NINAJITAHIDI KUBORESHA ILI TUWE PAMOJA. KARIBUNI!